Na mwandishi wetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemjulia hali kiungo wa timu ya Yanga, Pacome Zouzoua ambaye anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam.
Pacome aliumia katika mechi ya mwisho ya Ligi Kuu NBC kati ya Yanga na JKT Tanzania ambayo ilichezwa Juni 30, 2026 kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamhuyo na Yanga kutoka uwanjani na ushindi wa mabao 3-0.
Rais Samia alifika hospitalini hapo leo Jumatatu Julai 6, 2026 ambapo picha zilimuonesha akiwa karibu na kitanda cha Pacome ingawa haikuweza kufahamika mbali na kumpa pole nini kingine alichozungumza na mchezaji huyo.
Pacome alichezewa rafu na beki wa JKT Tanzania, Hassan Wahabi katika purukushani za kuwania mpira na mwamuzi kumpa beki huyo kadi ya njano kabla ya kuifuta na kumpa nyekundu.
Hali ya Pacome ilionekana kuwa mbaya kwani wakati akiwa chini akipatiwa huduma ya kwanza baadhi ya wachezaji walionekana wakiwa wamejishika vichwa hali iliyoashiria kushtuliwa na ukubwa wa majeraha aliyoyapata mchezaji huyo.
Baada ya Pacome kuumizwa, jioni ya siku hiyo picha zilimuonesha mchezaji huyo akiwa amefungwa bandeji kubwa mguuni hali iliyoashiria ukubwa wa tatizo lililompata.
Mbali na Rais Samia na wanamichezo mbalimbali, Wahabi naye alifika hospitalini hapo kumjulia hali Pacome.
Kimataifa Rais Samia amjulia hali Pacome
Rais Samia amjulia hali Pacome
Read also
