Riyadh, Saudi Arabia
Kocha wa zamani wa timu ya Tottenham Hotspur ya England, Ange Postecoglou ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya Al-Nassr ya Saudi Arabia.
Al-Nassr, timu ambayo pia anaichezea mwanasoka wa zamani wa timu za Real Madrid na Man United, Cristiano Ronaldo, kwa mara ya kwanza Mei mwaka huu ilifanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu Saudi Arabia maarufu Saudi Pro League.
Kabla ya kumteua Ange, Al-Nassr ilikuwa ikinolewa na kocha kutoka Ureno, Jorge Jesus lakini kocha huyo mwenye umri wa miaka 71, aliachana na klabu hiyo baada ya kumalizika kwa msimu uliopita.
Kwa kipindi kirefu Postecoglou amekuwa bila ya kazi yangu atimuliwe katika klabu ya Nottingham Forest Oktoba mwaka jana, timu ambayo aliinoa kwa siku zisizozidi 40.
Postecoglou, kocha mwenye umri wa miaka 60, raia wa Australia na mzaliwa wa Ugiriki, amesaini mkataba wa miaka miwili na Al-Nassr.
Moja ya mafanikio ya kukumbukwa na Postecoglou ni wakati akiwa na Spurs ambayo mwaka 2025 aliiwezesha kubeba taji la Europa Ligi lakini kabla ya hapo alikuwa Celtic ya Uskochi, timu ambayo aliiwezesha kutwaa taji ya ligi kuu nchini humo mara mbili.
Kwa siku za karibuni, Postecoglou amekuwa akifanya kazi ya uchambuzi wa mechi za soka kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 zinazoendelea katika nchi za Marekani, Canada na Mexico.
Kimataifa Postecoglou kocha mpya Al-Nassr
Postecoglou kocha mpya Al-Nassr
Read also
