Na mwandishi wetu
Kiungo mshambuliaji mpya wa Azam, Tape Edinho ameanza kuonesha makali yake kwenye kikosi hicho baada ya jana kutoa pasi iliyozaa bao katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Grand SC.
Edinho alitoa pasi hiyo kwa Prince Dube aliyeunganisha mpira huo uliojaa wavuni katika mchezo huo wa kujiandaa na msimu ujao wa 2022/23.
Azam kwa sasa imejichimbia El Guna, Misri ikiendelea na maandalizi yake hayo wakitarajia kumaliza kambi hiyo wiki ijayo ikiwa ni kwa siku 20 pekee kabla ya kurejea nchini kwa ajili ya Ligi Kuu ya NBC Bara.
Ushindi huo dhidi ya Grand unakuwa wa kwanza kwa Azam katika mechi hizo za kirafiki baada ya awali kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Wadi Degla.
Hata hivyo, uwezo unaooneshwa na Edinho katika kuunganisha timu hiyo eneo la ushambuliaji umeonekana kuwa dalili njema kwa kikosi hicho kilicho chini ya kocha Abdihamid Moallin ambaye anatajwa kuhusika kwa kiasi kikubwa katika usajili wa timu hiyo.
Azam itakayoanza mechi yake ya kwanza ya ligi dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam imeahidi kufanya makubwa msimu ujao wakitaka kufuta makosa ya msimu uliopita na kurejesha heshima yao kama ilivyoelezwa na mmiliki wa timu hiyo, Yusuf Bakhresa.
Soka Edinho atengeneza bao Azam
Edinho atengeneza bao Azam
Read also
