Na mwandishi wetu
Karia anafaa, Karia hafai, ni mjadala uliotawala ukimhusu Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia lakini hatimaye wanaomjadili wamepewa rasmi ruksa ya kumpinga kwenye sanduku la kura.
Mwanamichezo yeyote ambaye hajaridhishwa na uongozi wa Karia pale TFF huu ni wakati wake wa kujitokeza kumpinga katika uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo badala ya kuishia kumjadili.
TFF wametangaza uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo ambao umepangwa kufanyika Agosti 16, 2025 mkoani Tanga hivyo anayejiamini na ana sifa za kuchukua nafasi ya Karia amepewa ruksa hiyo.
Katika uchaguzi huo mbali na nafasi moja ya urais inayoshikiliwa na Karia, nafasi nyingine zitakazogombewa ni ujumbe wa kamati ya utendaji ambazo zipo nafasi sita.
Kwa mujibu wa taarifa ya TFF iliyopatikana Jumamosi hii Juni 14, 2025 na kusainiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Kiomoni Kibamba, fomu za kuwania nafasi hizo zitaanza kutolewa Jumatatu yaani Juni 16 2025 kwenye ofisi za TFF jijini Dar es Salaam na mwisho wa zoezi hilo ni Juni 20, 2025.
Kwa anayetaka nafasi ya urais atalazimika kulipa Sh 500,000 kwa ajili ya fomu hizo wakati wale wa ujumbe wa kamati ya utendaji kila fomu gharama yake ni Sh 200,000.
Soka TFF yatoa ruksa wanaotaka kumrithi Karia
TFF yatoa ruksa wanaotaka kumrithi Karia
Read also
