Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema ushindi walioupata Jumamosi hii dhidi ya KMC ni kiashiria tosha kwamba wamedhamiria kutetea taji lao la Ligi Kuu NBC kwa mara ya tatu mfululizo.
Ushindi huo wa mabao 3-0, umewafanya miamba hiyo kuzidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi wakifikisha pointi 43 katika michezo 16 huku wakifunga mabao 39.
“Pamoja na ushindi tulioupata lakini nimefurahi namna timu ilivyocheza na tulikuwa kwenye ubora ule tuliokuwa nao kabla ya mapumziko ya Afcon, kila mchezaji alijitoa, hiki ndio nataka kukiona katika kila mechi na ushindi huu unatupa nguvu ya kutimiza kusudio letu la kutetea taji,” alisema Gamondi.
Naye kocha mkuu wa KMC, Abdulhamid Moallin alifafanua: “Tumepoteza mbele ya timu bora Tanzania, tulijaribu kubadili mfumo wa uchezaji baadhi ya nyakati lakini ilishindikana.
“Yanga walituzidi kwenye maeneo mengi kiasi cha wachezaji wangu kukosa njia mbadala, tumekubali matokeo na tunarudi kujipanga kwa ajili ya mechi zinazokuja,” alisema Moallin.
Soka Gamondi awaza taji la 3 ligi kuu
Gamondi awaza taji la 3 ligi kuu
Read also