Pretoria, Afrika Kusini
Hatimaye Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini imeibuka kinara wa michuano mipya ya Ligi ya Soka Afrika (AFL) iliyozidunduliwa Oktoba 20 mwaka huu jijini Dar es Salaam baada ya kuibwaga Wydad Casablanca mabao 2-0.
Ushindi huo uliopatikana katika mechi ya fainali iliyochezwa leo Jumapili umeifanya timu hiyo ibebe taji hilo la michuano kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2 baada ya kulala kwa 2-1 katika mechi ya kwanza ugenini.
Mabao ya Mamelodi yalifungwa na Peter Shalulile na Aubrey Modiba yalitosha kuwafanya mashabiki wa timu hiyo watoke kwenye Uwanja wa Loftus Versfeld vifua mbele wakijivunia timu yao kuweka historia katika michuano hiyo mipya iliyoshirikisha timu nane.
Waydad ndio walioonesha dalili za kutoka na ushindi kwa namna ambavyo walikuwa wakiwasumbua wapinzani wao kwa kupeleka mashambulizi ya mapema ambayo hata hivyo hayakuzaa matunda.
Mwisho wa yote walikuwa ni Mamelodi walioweka historia kwa kuwa timu ya kwanza kubeba taji la michuano hiyo iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam huku ikitoa dalili zote za kuwa mashindano makubwa ya klabu barani Afrika na yenye utajiri.
Uzinduzi wa michuano hiyo ulihudhuriwa na marais wa Fifa, Giani Infantino na wa CAF, Patrice Motsepe na wanamichezo wengine maarufu akiwamo kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger na wengineo.
Kimataifa Mamelodi wabeba taji la AFL
Mamelodi wabeba taji la AFL
Read also