Manchester, England
Kocha wa zamani wa Man United aliyepata mafanikio makubwa na timu hiyo, Sir Alex Ferguson amefiwa na mkewe Cathy Ferguson (pichani) ambaye umauti umemkuta akiwa na miaka 84.
“Kila mmoja hapa Manchester United anatuma salamu za rambirambi kwa Sir Alex Ferguson na familia yake kutokana na kifo cha Mama Cathy,” ilisema taarifa ya klabu hiyo.
“Mama Cathy alikuwa mke mpendwa, mama, dada, bibi na nguzo imara kwa Sir Alex katika kipindi chote akiwa kocha,” ilifafanua taarifa hiyo na kuongeza kwamba kwa heshima ya marehemu wachezaji watavaa vitambaa maalum katika mechi na Brentford.
Sir Alex Ferguson alistaafu kuifundisha Man United mwaka 2013 baada ya kuwa kocha wa timu hiyo kwa zaidi ya miaka 26 na uamuzi wa kustaafu aliuchukua ili apate muda zaidi wa kuwa na Cathy na familia yake.
Awali Ferguson alitaka kustaafu kuifundisha timu hiyo kabla ya mwaka 2013 lakini alikuwa ni Cathy aliyemshauri asichukue uamuzi huo mapema.
Kimataifa Mke wa Ferguson afariki dunia
Mke wa Ferguson afariki dunia
Related posts
Read also