London, England
Kila kitu kilikwenda vizuri, kiungo Paul Pogba alikuwa akisubiriwa kuondoka Man United na kutua Man City lakini ghafla akabadili mawazo, akaikataa City akidaiwa kuwahofia mashabiki wanazi wa United.
Mkataba wa Pogba na United umebakisha wiki chache kabla mchezaji huyo kuwa huru na mwelekeo ulikuwa ni City lakini baada ya Pogba kuikataa City bila shaka klabu za Juventus, PSG na Real Madrid ni kati ya timu zinazodaiwa kutaka huduma ya Pogba na bila shaka atakuwa na kazi ya kuchagua moja ya timu hizo na nyinginezo zinazofuatilia hatima ya mchezaji huyo.
Awali ni City walioonyesha nia ya kumpata mchezaji huyo na kwa kuwa Fernandinho anaondoka City na hivyo kocha Pep Guardiola atahitaji mtu mwingine wa kuongezea nguvu katika safu ya kiungo na Pogba alionekana mtu sahihi wa kuziba pengo hilo na inadaiwa walishakubaliana kila kitu kuhusu maslahi binafsi ya mchezaji huyo.
Pogba ameamua kubadili uamuzi na kuikata City inayotumia jezi za bluu akitambua uamuzi wa kujiunga na timu hiyo jirani unaweza kumuweka katika wakati mgumu mbele ya mashabiki wa United ambao hawatapenda kuona akiichezea timu hiyo mahasimu wao wa jiji la Manchester.
Carlos Tevez ni mchezaji wa mwisho ambaye aliachana na jezi nyekundu ya United takriban miaka 10 iliyopita na kuvaa ya bluu, uhamisho ambao uliibua utata miongoni mwa mashabiki na hapana shaka uamuzi wa Pogba nao unaweza kumuweka pagumu zaidi mchezaji huyo iwapo ataamua kuachana na jezi nyekundu na kuvaa ya bluu.
Kimataifa Pogba aikataa Man City
Pogba aikataa Man City
Related posts
Read also