Na mwandishi wetu
Klabu ya Yanga imeeleza kukamilika kwa dili la Clara Luvanga aliyetimkia Dux Logrono ya Hispania, ni mwanzo wa wachezaji wengi watakaowauza hivi karibuni kutoka timu yao ya wanawake ya Yanga Princess.
Clara aliyevuma akiwa na kikosi cha timu ya U17 ya Tanzania kwenye fainali za Kombe la Dunia India 2022, amejiunga na Dux inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kwa mkataba wa miaka mitatu.
Mkurugenzi wa Mashindano Yanga, Saad Kawemba alisema wanafurahia kuwa na maendeleo ya namna hiyo katika klabu akisisitiza kuwa wapo wachezaji wengi wa Princess ambao wameshafanyiwa mipango na muda si mrefu wataweka wazi wanakoelekea nyota wao hao.
“Ni maendeleo kwa kweli na ni jambo jema kwa klabu, tuna idadi ndefu kidogo kuhusu uhamisho wa wachezaji wetu kwenda nje na hivi karibuni klabu itatoa taarifa rasmi kuhusiana na hilo.
“Nasema hivyo kwa sababu orodha ni ndefu kidogo ndio maana klabu itatoa taarifa rasmi kwa wanaoondoka, ni mipango mikubwa tuliyonayo kuhusiana na hilo na muda si mrefu itawekwa wazi,” alifafanua Kawemba.
Timu ya Dux Logrono ina miaka 15 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2008 kabla ya Julai Mosi, mwaka juzi kuuzwa kwa Dux Gaming ambapo washirika wake ni DJ Mariio na kipa wa Real Madrid, Thibaut Courtois.
Timu hiyo kwa sasa inanolewa na Gerardo Leon, beki wa zamani wa timu za Villarreal, Valencia na Real Sociedad za Hispania.
Soka ‘Clara Luvanga ni mwanzo tu’
‘Clara Luvanga ni mwanzo tu’
Read also