Na mwandishi wetu
Klabu ya KMC imetangaza kuwanasa mshambuliaji Ibrahim Elias kutoka Kibra FC ya Kenya na kocha msaidizi John Matambala ambaye hapo kabla alikuwa kocha msaidizi Azam FC.
KMC imewatangaza wawili hao kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii ambapo Elias raia wa Somalia ameelezwa kupewa mkataba wa miaka miwili na timu hiyo yenye maskani yake Kinondoni, Dar es Salaam.
Matambala anaungana na bosi wake wa zamani, Msomali Abdihamid Moalin ambaye naye amejiunga na KMC hivi karibuni akitokea Azam kuchukua mikoba ya Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.
Na Azam imemuaga Matambala aliyehudumu kwenye nafasi mbalimbali akiwa katika klabu hiyo kabla ya kuwa kocha msaidizi, ikieleza kumshukuru na kumtakia kila la heri kwenye majukumu yake hayo mapya.
Wachezaji wengine waliojiunga na KMC mbali na Elias ni Vincent Abuu aliyetokea Coastal Union, Juma Shemvuni (Mbeya City), Andrew Simchimba (Ihefu) na kipa Wilbol Maseke aliyekuwa Azam.
Soka Kocha Azam atua KMC
Kocha Azam atua KMC
Read also