
New York, Marekani
Mrembo Kim Kardashian ni kama vile amekolea kwa penzi la dogo, Pete Davidson na sasa anataka kuanza maisha mapya na dogo huyo kwa kuhakikisha wanapata mtoto.
Kim mwenye umri wa miaka 41 na Pete mwenye miaka 28 wamekuwa pamoja kwa kipindi cha miezi saba na sasa kinachoonekana ni kwamba penzi lao linazidi kuwa moto na hivyo haishangazi kusikia Kim akifikiria kupata mtoto na Pete.

Habari za Kim kutaka kupata mtoto na Pete ni dhahiri zinaweza kushangaza wengi hasa baada ya awali kuwapo habari kwamba mwanadada huyo alikataa mpango wa kuzaa na kwamba watoto wanne wa kwenye ndoa yake na Kanye West ambayo imesambaratika wanamtosha.
Penzi la Kim na Pete linazidi kupamba moto, katika siku za karibuni wameonekana pamoja katika matukio mbalimbali huku kila mmoja akionyesha anavyomkubali mwenzake, Kim pia aliwahi kuonekana akiwa na familia ya Pete jambo lililotoa kila dalili za wawili hao kuwa wapenzi walioshibana.
Kim alifunga ndoa na Kanye mwaka 2014 lakini ndoa iliingia katika sintofahamu na kuvunjika rasmi mapema mwaka huu, kabla ya hapo aliolewa na Damon Thomas mwaka 2000 na kuachana mwaka 2004 kisha akaolewa na Kris Humphries mwaka 2011 na kuachana rasmi mwaka 2013.