Na mwandishi wetu
Kiungo mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama ameibuka kidedea na kuwa mchezaji bora wa wiki wa mechi ya nne ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ushindi huo wa Chama ulitangazwa usiku wa kuamkia leo Jumatano na Shirikisho la Soka Afrika (Caf), akiwabwaga Walid Sabar wa Raja Casablanca, Peter Shalulile wa Mamelodi Sundowns na Ahmed Zizo wa Zamalek.
Chama raia wa Zambia alipata ushindi huo kutokana na kura zilizokuwa zikipigwa kwa takriban siku tatu mfululizo kwenye ukurasa rasmi wa michuano hiyo wa mtandao wa kijamii wa Twitter.
Kiungo huyo alishinda kwa kura asilimia 68.7, Shalulile akipata asilimia 14.9 wakati Sabbar akiokota kura 10.9% na Zizo akiambulia 5.6%.
Licha ya wachezaji wengine kuonesha kiwango kuzisaidia timu zao kupata ushindi kwenye mechi za wiki ya nne lakini Chama alielezwa kuonesha kiwango bora zaidi katika mchezo wao dhidi ya Vipers na kufunga bao pekee la ushindi kwenye mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Pia, Chama alijumuishwa kwenye mabao matano bora yaliyofungwa wiki hiyo, yumo kwenye kikosi bora cha wiki sanjari na beki wa kulia wa Wekundu hao, Shomari Kapombe.
Soka Chama kidedea CAF
Chama kidedea CAF
Read also