Na mwandishi wetu
Siku mbili tangu timu ya Singida Big Stars itangaze kuachana na mshambuliaji, Peu Da Cruz, juzi, mchezaji huyo ametambulishwa kujiunga na timu ya Nautico Marcilio inayoshiriki Ligi Daraja la Nne nchini Brazil.
Nautico ilimtambulisha Cruz raia wa Brazil wakieleza kuwa kijana wao amerejea nyumbani baada ya kuzunguka timu kadhaa huko Mexico, Poland, Ureno, Tanzania na kadhalika akiwa na uzoefu mkubwa wa kuwasaidia.
Hata hivyo, muda mchache kabla ya utambulisho huo, Cruz raia wa Brazil alieleza hisia zake na kuishukuru Singida BS kwa muda wote alioitumikia timu hiyo na kumtimizia ndoto zake.
“Nimemaliza safari yangu ya soka na Singida Big Stars, nashukuru kwa kuamini kazi yangu, mashabiki kwa upendo wote ambao wamenionesha kwa miezi yote nilipokuwa naitumikia timu hii nzuri.
“Kucheza Ligi Kuu barani Afrika umekuwa ni uzoefu wa kipekee ambao nitaendelea kuishi nao milele. Daima nitawafurahia na kuwakumbuka, asante sana Singida,” aliandika Cruz kwenye ukurasa wake wamtandao wa Instagram.
Singida ilieleza kuachana na Cruz kutokana na sababu za kifamilia alizokuwa nazo mchezaji huyo hukuikimtakia kila heri aendako.
LigiKuu Da Cruz aibukia Brazil
Da Cruz aibukia Brazil
Related posts
Read also