Doha Qatar
Kocha wa Ureno, Fernando Santos amekiri kukerwa na nyota wake Cristiano Ronaldo kwa kitendo cha mchezaji huyo kumtamkia maneno yasiyopendeza baada ya kutolewa katika mechi dhidi ya Korea Kusini na sasa haijulikani kama atampanga leo Jumanne katika na Switzerland.
Ureno, inaumana na Switzerland katika mechi ya kuwania tiketi ya robo fainali huku kocha Santos akikataa kuthibitisha kama atampanga mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 au la.
Ronaldo alionekana kujawa hasira baada ya Santos kumtoa dakika ya 65 katika mechi ambayo Ureno ililala kwa mabao 2-1 na baadaye kamera kumuonyesha mchezaji huyo akiwa mwenye hasira na kumtamkia kocha wake kwa kumwambia, ‘ana haraka ya kumfanyia-sub (kumtoa)’.
Katika tukio hilo hilo, Ronaldo pia wakati akitoka uwanjani aliingia katika mzozo wa maneno na mchezaji wa Korea Kusini, Cho Gue-Sung na ni baada ya mechi hiyo ndipo Santos alipobaini kwamba Ronaldo alikerwa na kudhihirisha hasira zake baada ya kutolewa na kocha huyo.
“Ngoja nigawanye majibu haya katika makundi mawili,” alisema Santos alipoulizwa kuhusu picha za video zilizomuonyesha Ronaldo akionyesha wazi kuchukizwa na hatua ya kocha wake kumtoa.
“Mara tu baada ya mechi nilizungumza katika mahojiano ya haraka na baada ya hapo nikaenda kwenye mkutano na waandishi na hapo nilisema kitu ambacho nakirudia, sikusikia chochote, nilikuwa mbali na ndio maana niliona akijibizana na mchezaji wa Korea, si zaidi ya hilo,” alisema Santos.
“Na sasa je nimeshaangalia picha za video, ndio, na sijapenda alichokifanya, sijapenda kabisa na baada ya hapo linakuwa jambo la ndani, litafanyiwa kazi, sasa ninachofikiria ni mechi ijayo, kila mmoja akili yake ipo kwenye mechi,” alisema Santos.
Ronaldo baada ya tukio hilo pia alisema kwamba mchezaji wa Korea alimkaripia akimtaka atoke haraka uwanjani na yeye kumjibu kwa hasira akimtaka anyamaze kwani hana mamlaka.
Mechi za leo Jumanne Kombe la Dunia
Morocco v Hispania
Ureno v Switzerland
Kimataifa Ronaldo amkera kocha Ureno
Ronaldo amkera kocha Ureno
Related posts
Read also