Na mwandishi wetu
Klabu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro imetangaza kuvunja mkataba na kocha wao wa makipa, Razak Siwa na tayari kocha huyo wa zamani wa Yanga ameondoka kunako klabu hiyo na kurudi kwao nchini Kenya.
Mtibwa iliingia mkataba wa mwaka mmoja na Siwa mwanzoni mwa msimu huu baada ya Yanga kuachana na kocha huyo wa zamani wa Bandari FC ya Kenya ambaye pia amewahi kuwanoa makipa wa timu ya Taifa ya Kenya, Harambee Stars.
Aidha, ingawa Mtibwa hawakutaka kuweka wazi sababu za msingi za kuchana na Siwa lakini duru mbalimbali zimefafanua ni kutokana na uongozi wa timu hiyo ya Morogoro kutoridhishwa na uwezo wa kocha huyo.
Akizungumzia taarifa hiyo leo, Msemaji wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru alisema kwamba baada ya mazungumzo marefu na kocha huyo aliyekuwa amebakisha miezi kadhaa kumaliza mkataba wake wamekubaliana kuachana.
“Uongozi wa Mtibwa Sugar ulikuwa kwenye mazungumzo na Siwa na kukubaliana kuvunja mkataba. Kwa sasa tunasaka kocha mwingine tutakayeendelea naye kuwanoa makipa wetu,”alisema.
Soka Mtibwa yaachana na Siwa
Mtibwa yaachana na Siwa
Related posts
Read also