Manchester, England
Beki wa klabu ya Manchester City aliyesimamishwa, Benjamin Mendy amekana tuhuma nyingine za ubakaji zinazomkabili katika mahakama ya Chester Crown.
Mendy mwenye umri wa miaka 28 sasa anakuwa amekana kuhusika katika makosa manane ya ubakaji, moja la udhalilishaji kijinsia na moja la kuwa na dhamira ya kubaka, matukio anayodaiwa kuwafanyia wanawake saba nyumbani kwake kati ya Oktoba 2018 na Agosti 2021.
Mtu mwingine anayehusika katika kesi hiyo ni Louis Saha Matturie mwenye umri wa miaka 40 ambaye naye kama Mendy amekana kuhusika katika mashitaka hayo wakati kesi yao ikitarajiwa kuanza kusikilizwa Jumatatu.
Mendy aliyejiunga na Man City mwaka 2017 akitokea Monaco na kuichezea timu hiyo mechi 50 za Ligi Kuu England, mara tu baada ya kuhusishwa na tuhuma hizo alijikuta akisimamishwa na timu yake ingawa kwa sasa yeye na mwenzake wapo nje kwa dhamana.
Kimataifa Mendy akana tena kubaka
Mendy akana tena kubaka
Read also