London, England
Baada ya Liverpool kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Man City katika mechi ya Ngao ya Jamii Jumamosi hii, kocha wa Jurgen Klopp amesema amevutiwa na kiwango cha mshambuliaji wake mpya, Darwin Nunez.
Mshambuliaji huyo kutoka Uruguay aliingia uwanjani zikiwa zimebaki dakika 30 kabla ya mpira kumalizika lakini alitumia vizuri muda huo na kumfanya kocha wake kujivunia usajili wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 aliyemsajili kotoka Benfica ya Ureno kwa ada inayotajwa kuwa huenda ikafikia zaidi ya Euro 80 milioni.
Nunez alikuwa kama ndiye aliyebadili mchezo, kwani alianza kwa kusababisha penalti katika bdakika ya 83, timu hizo zikiwa sare ya bao 1-1, penalti ambayo Mohamed Salah aliitumia kuipatia Liverpool bao la pili na hivyo ubao kusomeka 2-1 kabla Nunez hajamalizia kwa kufunga bao la tatu kwa kichwa katika dakika za nyongeza na kuifanya Liverpool itoke uwanjani na ushindi huo wa 3-1.
Liverpool ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 21 lililofungwa na Alexander-Arnold na City kusawazisha dakika ya 71 mfungaji akiwa ni Alvarez na baada ya hapo ndipo Nunez alipofanya mambo yaliyomvutia Klopp hadi kumfanya ajivunie usajili wa mchezaji huyo.
Ushindi huo una maana kubwa kwa Liverpool ambao msimu uliopita wa 2021/22 walishuhudia ndoto yao ya kutwaa mataji manne ikiota mbawa na badala yake kuishia na mataji mawili ya FA na Ligi huku taji la Ligi ya Mabingwa wakishindwa kulibeba mbele ya Real Madrid walipolala kwenye mechi ya fainali wakati la Ligi Kuu England walilipoteza mbele ya Man City kwa tofauti ya pointi moja.
Kwa maana hiyo ushindi wa Ngao ya Jamii ambao ni wa kwanza kwa timu hiyo tangu mwaka 2006, unakuwa ni mwanzo mpya wa timu hiyo kwa msimu wa 2022/23 kutimiza ndoto ambazo ziliwaponyoka katika msimu wa 2021/22 licha ya matarajio makubwa waliyokuwa nayo.
Mara tu baada ya kuingia Nunez alianza mapema kumpa changamoto kipa wa Man City, Ederson kabla ya kutengenza penalti iliyozaa bao lakini pia alimfanya kipa huyo kufanya kazi ya ziada kuzuia mpira uliopigwa na Nunez ambao pia ungeweza kuipa Liverpool bao.
“Alikuwa vizuri, vizuri hasa, ni jambo lililo wazi kwamba atakuwa vizuri zaidi siku hadi siku, tunaishi katika dunia ambayo kila mtu anafanyiwa tathmini anapoonekana mara ya kwanza na hilo linaweza lisiwe jambo zuri kwa kila mtu lakini huwa linatokea mara kwa mara,” alisema Klopp.
Kimataifa Klopp ampa tano Nunez
Klopp ampa tano Nunez
Related posts
Read also