Na mwandishi wetu
Wachezaji 30 wa timu ya soka ya wanawake ya Tanzania ‘Twiga Stars’ wakiwamo 10 wanaocheza soka nje ya nchi wametangazwa rasmi leo Jumamosi, Mei 10, 2025.
Kikosi hicho chini ya kocha Bakari Shime (pichani) ni kwa ajili ya maandalizi ya mechi za kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrrika (Wafcon) kwa wanawake pamoja na mechi nyingine za kwenye kalenda ya Fifa.
Katika orodha ya wachezaji hao iliyopatikana kwenye vyanzo vya habari vya TFF, wachezaji wanaocheza soka nje ya Tanzania ni Aisha Masaka ambaye anaichezea Brighton and Holves Albion inayoshiriki ligi ya wanawake England.
Wengine timu na nchi wanazocheza soka katika mabano ni pamoja na Enekia Kasonga (Mazatlan FC) Juletha Singano (Juarez) na Opa Clement (Juarez) ambao wote wanacheza nchini Mexico.
Noela Luhala (Asa Tel Aviv ya Israel), Clara Luvanga (Al Nasr FC ya Saudi Arabia) pamoja na Diana Lucas (Trabzonspor ya Uturuki).
Wengine ambao wanacheza soka katika klabu tofauti za nchini Misri ni Hasnat Ubamba (FC Masr), Suzan Adam (Tutankhamun) na Maumina Kaimu (ZED FC).
Wachezaji wanaocheza klabu za ndani ni Najat Abbas (JKT Queens), Asha Mrisho (Mashujaa Queens), Janet Shija (Simba Queens), Nusrat Khamis (Alliance Girls) na Fatuma Issa (Simba Queens).
Wengine ni Asha Ramadhan (Yanga Princess), Lydia Maxmilian (JKT Queens), Vaileth Nicholaus (Simba Queens), Donisia Minja (JKT Queens), Esther Maseke (Bunda Queens) na Anastazia Katunzi (JKT Queens).
Wachezaji wengine ni Agness Palangyo (Yanga Princess), Christer Bahera (JKT Queens), Aisha Mnuka (Simba Queens), Janeth Christopher (JKT Queens) na Elizabteh Chenge (JKT Queens).
Wengine ni Stumai Abdallah (JKT Queens), Winifrida Gerald (JKT Queens), Mary Siyame (Fountain Gate Princess) na Jamila Rajab (JKT Queens).
Katika Kikosi kilichotangazwa Februari mwaka huu, wachezaji 11 wanaocheza nje ya Tanzania waliitwa lakini safari hii amewaita 10 huku jina la Malaika Meena wa Bristol City ya England likikosekana.
Kimataifa Mastaa 10 wa nje waitwa Twiga Stars
Mastaa 10 wa nje waitwa Twiga Stars
Read also