Na mwandishi wetu
Kocha wa Yanga, Miloud Hamdi (pichani) amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi Aprili huku mshambuliaji wa Dodoma Jiji, Iddi Kapwagile akiibuka mchezaji bora wa mwezi huo.
Taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) iliyopatikana kwenye mitandao ya kijamii ilimtaja Kipwagile kuwa ameibuka kinara wa tuzo hiyo kwa kuonesha mwendelezo wa kiwango bora.
Katika uteuzi wa kuwania tuzo hiyo uliofanywa na kamati ya tuzo ya TFF, Kipwagile alikuwa akichuana na Pacome Zouzoua wa Yanga pamoja na Haruna Chanongo wa Tanzania Prisons.
Kipwagile alitoa mchango mkubwa katika michezo minne ya Dodoma Jiji, akiifungia timu hiyo mabao matatu na kuhusika katika mengine matatu huku akicheza jumla ya dakika 320.
Kuhusu Mohdi yeye aliingia katika kuwania tuzo hiyo na makocha Amani Josiah wa Tanzania Prisons pamoja na David Ouma wa Singida Black Stars.
Mohdi aliwashinda wenzake baada ya kuiongoza vyama Yanga kushinda michezo yote minne ambayo walicheza mwezi Aprili na kuendelea kujiimarisha kileleni wa msimamo wa Ligi Kuu NBC.
Katika mechi hizo za ushindi Yanga iliwafunga Azam FC mabao 2-1, Coastal Union 1-0, Tabora United 3-0 na Fountain Gate 4-0.
Kamati ya tuzo pia imemchagua meneja Uwanja wa Ismhuyo, Ashraf Omar kuwa meneja bora wa uwanja wa mwezi Aprili kwa namna ambavyo amesimamia vyema miundombinu ya uwanja na usimamizi wa mambo mengine yahusuyo uwanja huo uliopo jijini Dar es Salaam.
Kwenye Ligi ya Championship, Emmanuel Maziku wa Stand United ameibuka mchezaji bora wa ligi hiyo kwa mwezi Aprili akiwa amefunga mabao manne katika dakika 194 alizocheza kwa mwezi wote wa Aprili.
Maziku katika kinyang’anyiro hicho amewashinda Mohammed Hassan wa Transit Camp na Ramadhan Kapalamoto wa Songea United alioingia nao fainali.
Katika Ligi ya Championship pia kocha Ramadhan Ahmada wa Transit Camp ameteuliwa kuwa kocha bora wa mwezi Aprili kwa kuiongoza vyema timu hiyo kwa kipindi hicho akiwashinda Malale Hamsin wa Mbeya City na Awadh Juma wa Mtibwa Sugar.
Kimataifa Hamdi kocha bora Aprili
Hamdi kocha bora Aprili
Related posts
Read also