Na mwandishi wetu
Simba ya Tanzania sasa itaumana na RS Berkane ya Morocco katika mechi ya fainali ya kuwania Kombe la Shirikisho Afrika.
Simba na Berkane zote zimesonga mbele baada ya matokeo ya mechi zao za nusu fainali zilizochezwa jana Jumapili Aprili 27 timu hizo zikiwa kwenye viwanja vya ugenini. Walianza Simba kucheza saa 10 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki na kufuatiwa na mechi ya Berkane na CS Constantine ya Algeria iliyopigwa saa moja usiku.
Simba imeitoa Stellenbosch kwa bao 1-0, ushindi ilioupata katika mechi ya kwanza lakini jana ikiwa ugenini timu hiyo ilifanikiwa kulazimisha sare ya 0-0.
Kwa upande wa Barkane imeitoa CS Constantine ya Algeria kwa jumla ya mabao 4-1, jana ilifungwa bao 1-0 ikiwa ugenini lakini katika mechi ya awali ikiwa nyumbani ilishinda kwa mabao 4-0.
Simba itaumana na Berkane, timu ambayo inasaka taji la tatu katika michuano ya klabu barani Afrika wakati Simba wanapambana kuweka historia kwa kubeba kwa mara ya kwanza taji lenye hadhi hiyo.
Mara ya mwisho Simba kufikia hatua ya fainali ya michuano ya klabu barani Afrika ilikuwa mwaka 1993 lakini ilishindwa kutamba mbele ya Stella ya Ivory Coast.
Kimataifa Ni Simba, Berkane fainali Shirikisho Afrika
Ni Simba, Berkane fainali Shirikisho Afrika
Read also