Manchester, England
Kocha wa Man United, Erik ten Hag amemtaka mshambuliaji wake, Marcus Rashford kuhakikisha anafunga mabao mengi msimu huu baada ya kuandamwa na ukame wa mabao kwa miezi sita.
Rashford jana Jumamosi alifunga bao dhidi ya Southampton katika ushindi wa 3-0, bao ambalo limekuja baada ya mchezaji huyo kutoka uwanjani bila kufunga katika mechi 13 za Man United.
Mara ya mwisho, Rashford kuifungia bao Man United ilikuwa Machi 9 mwaka huu katika mechi dhidi ya Everton, mechi ambayo timu hiyo ilitoka na ushindi wa mabao 2-0.
Kutokana na ukame wa mabao ambao umekuwa ukimuandama Rashford, 26, kuna wakati alijikuta akishambuliwa vikali na mashabiki wa Man United wengi wao wakimshutumu kwa kutojituma.
Kabla ya mechi na Sothampton Ten Hag aliulizwa ni kwa nini alimpanga Rashford kikosi cha kwanza ambapo kocha huyo alisema kwamba mshambuliaji huyo alihitaji kufunga bao moja au kutoa asisti ili arudi katika kasi yake ya mabao.
Matumaini ya Ten Hag ni kwamba mshambuliaji huyo kwa sasa ni kama amefungua njia baada ya rekodi mbaya ya mabao manane tu kwa mashindano yote ya msimu uliopita wa 2023-24, hiyo ni baada ya kuwa na rekodi ya kuvutia ya mabao 30 kwa msimu wa 2022-23.
“Hilo ni jambo muhimu kwa kila mshambuliaji, wanachohitaji ni kuwa katika orodha ya waliofunga, baada tu ya bao la kwanza mengine mengi yanafuata,” alisema Ten Hag.
Kimataifa Ten Hag amtaka Rashford atupie kwa wingi
Ten Hag amtaka Rashford atupie kwa wingi
Read also