Na mwandishi wetu
Kocha wa Simba, Davids Fadlu na kiungo wa timu hiyo, Jean Ahoua wameibuka vinara wa tuzo za soka za Ligi Kuu NBC kwa mwezi wa Agosti kwa kutwaa tuzo ya kocha na mchezaji bora.
Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania iliyopatikana leo Jumatatu, Fadlu na Ahoua wamebeba tuzo hizo kutokana na mafanikio ya Simba katika mechi mbili za ligi hiyo zilizochezwa mwezi Agosti.
Katika mechi hizo Ahoua aliifungia Simba bao moja na kuhusika katika mengine matatu wakati Simba ikiichapa Tabora United mabao 3-0 na kuichapa Fountain Gate mabao 4-0.
Naye Fadlu ametwaa tuzo ya kocha bora akiwashinda Patrick Aussems wa Singida Black Stars na Abdallah Hussein wa Mashujaa ambao aliingia nao katika fainali ya kinyang’anyiro hicho.
Kocha Fadlu ambaye huu ni msimu wake wa kwanza na Simba, aliiongoza timu yake kutopoteza mchezo hata mmoja na kukusanya pointi sita na mabao saba ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.
Naye Ashraf Omar ambaye ni meneja wa Uwanja wa Meja Jeneral Isamuhyo ameshinda tuzo ya meneja bora wa mwezi kwa kufanya vizuri katika usimamizi wa matukio na miundombinu ya uwanja huo.
Soka Fadlu, Ahoua wang’ara Agosti
Fadlu, Ahoua wang’ara Agosti
Read also