Istanbul, Uturuki
Beki wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Novatus Dismas Miroshi amejiunga na klabu ya Goztepe SK inayoshiriki Ligi Kuu Uturuki kwa mkataba wa miaka minne.
Miroshi ambaye ni mmoja wa wachezaji tegemeo katika kikosi cha Taifa Stars akiwa na rekodi ya kuichezea timu hiyo mara 22, alitangazwa rasmi na klabu hiyo Jumanne hii usiku.
“Tuna furaha kutagaza kumsajili Novatus Miroshi kwa mkataba wa miaka minne, tunamkaribisha kwa furaha Novatus na tunamtakia kila la heri katika safari yake kwenye mafanikio ya klabu yetu,” ilieleza taarifa ya Goztepe.
Kabla ya kujiunga na Goztepe, Miroshi alikuwa akiichezea klabu ya Shakhatar Donetsk ya Ukraine kwa mkopo akitokea klabu ya Zulte Waregem FC ya Ubelgiji.
Akiwa Shakhtar, Miroshi aliiwakilisha timu hiyo kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na pia alikuwa na kikosi cha Taifa Stars kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) zilizofanyika mapema mwaka huu nchini Ivory.
Kabla ya Miroshi, Mtanzania mwingine aliyecheza soka nchini Uturuki ni Mbwana Samatta ambaye alikuwa akiichezea klabu ya Fenerbahçe kati ya mwaka 2020 na 2021.
Kimataifa Miroshi asajiliwa Goztepe ya Uturuki
Miroshi asajiliwa Goztepe ya Uturuki
Related posts
Read also