Na mwandishi wetu
Kinara wa mabao Ligi Kuu NBC, Stephane Aziz Ki ameibua sintofahamu mitandaoni baada ya kuwashukuru mashabiki, wachezaji wenzake na wadau wengine wa timu hiyo.
Aziz Ki ameshukuru kwa muda wote wa msimu huu kwa namna walivyopambana na kuaminiana ingawa salamu hizo baadhi ya mashabiki wamezipa tafsiri ya kuwa mchezaji huyo anawaaga.
Kiungo huyo mshambuliaji raia wa Burkina Faso ameeleza hayo leo Jumatano katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram na kufafanua hisia zake katika kufanikisha ndoto zake.
“Kila kitu kiliwezekana, shukrani kwenu wachezaji wenzangu, wafanyakazi, kamati ya rais na hasa nyinyi mashabiki, wapendwa wangu, familia na pia kwa baraka za Mungu mwema kwa mara nyingine tena asante kwa uaminifu wako, msaada wako, imani yako, umenipa mengi katika msimu wote,” aliandika Aziz aliyefunga mabao 21.
Hata hivyo, andiko hilo kidogo liliibua sintofahamu kwa baadhi ya mashabiki wakihoji namna anavyotoa asante ni kama anataka kuihama timu hiyo.
Punde, Aziz alijibu ‘comment’ hizo na kufafanua: “Nawashukuru kwa sababu ni jambo dogo sana ninaloweza kufanya kuwashukuru nyinyi ambao mnanisaidia kila siku, haimaanishi kwaheri, niko hapa msijali.”
Soka Aziz Ki aibua sintofahamu
Aziz Ki aibua sintofahamu
Read also