London, England
Juhudi za Man City kuisaka saini ya Erling Haaland hatimaye zimezaa matunda baada ya mchezaji huyo kusaini kuichezea timu hiyo hii leo.
Haaland, mshambuliaji wa kimataifa wa Norway anajiunga na City kwa ada ambayo kwa mujibu wa habari zilizopatikana mwezi iliopita inadaiwa kufikia Dola 64 milioni ingawa City wenyewe hawajawa tayari kuthibitisha kiwango halisi cha fedha za usajili wa mchezaji huyo aliyekuwa akiichezea Borussia Dortmund ya Ujerumani.
Straika huyo amekuwa akisakwa na klabu kadhaa za Ulaya zikiwamo Real Madrid na Bayern Munich na hivyo City wana kila sababu ya kujivunia kumpata baada ya kuwashinda vigogo wenzao wa Ulaya katika kusaka saini ya Haaland.
Haaland alijiunga na Dortmund Januari 2020 akitokea Red Bull Salzburg na ameifungia timu hiyo mabao 41 katika mechi 41 kwenye msimu wake wa kwanza kucheza wote wakati katika timu ya Taifa ya Norway amefunga mabao 20 katika mechi 21 tangu aanze kuichezea timu hiyo mwaka 2019.
Tangu kuondoka kwa Sergio Aguero aliyetimkia Barcelona, City wamekuwa wakihaha kupata mshambuliaji wa hadhi yake hasa baada ya kuondoka akiweka rekodi ya mabao 254 katika klabu hiyo na sasa Haaland ambaye ndio kwanza ana miaka 21 anasubiriwa kwa hamu kuimarisha safu ya ushambuliaji ya City.
“Hii ni siku ya kujivunia kwangu na familia yangu, nimekuwa wakati wote nikiwaangalia City na nimekuwa nikipenda kufanya hivyo katika misimu ya karibuni, huwezi kufanya kitu lakini napendezewa na staili ya uchezaji wao, inavutia na wanatengeneza nafasi nyingi jambo ambalo ni sahihi kwa mchezaji kama mimi,” alisema Haaland.
“Kuna wachezaji wengi wa hadhi ya juu duniani katika kikosi na Pep ni mmoja wa makocha wazuri, kwa hiyo naamini niko katika sehemu nzuri ya kutimiza matakwa yangu, nataka kufunga magoli, kushinda mataji na kuboresha soka langu na naamini nitafanya hivyo nikiwa hapa,” aliongeza Haaland.
Kimataifa Haaland asaini Man City
Haaland asaini Man City
Related posts
Read also