Na mwandishi wetu
Simba imeongeza pointi tatu muhimu katika mbio za kuchuana na Azam FC kuisaka nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu NBC baada ya kuilaza Dodoma Jiji bao 1-0, mechi iliyopigwa Ijumaa hii kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Ushindi huo hata hivyo unaifanya Simba kuendelea kushikacnafasi ya tatu ikiwa na pointi 60 sawa na Azam inayoshika nafasi ya pili ikiwa pia na pointi 60 ingawa imeizidi Simba kwa wastani wa mabao, timu zote zikiwa zimecheza mechi 27.
Aliyepeleka kilio kwa Dom Jiji waliokuwa nyumbani ni mshambuliaji Freddy Koublan katika dakika ya saba ya mchezo huo akimalizia pasi ya winga, Edwin Balua.
Kwa upande wa Dom Jiji, matokeo hayo yanawafanya waendelee kubaki katika nafasi ya 11 wakiwa pia wamecheza mechi 27 katika ligi hiyo yenye timu 16 huku mbili zikisubiri kushuka daraja.
Dom Jiji pamoja na kuwa nafasi ya 11 lakini ina kazi ya kupambana katika mechi tatu zilizobaki ili kujiondoa katika hali hatarishi ya kushuka daraja na kucheza Championship msimu ujao.
Timu hiyo ya Dodoma pia isipoangalia inaweza kujikuta ikilazimika kucheza mechi za play off ili kuwania kubaki katika ligi hiyo msimu ujao.
.
Soka Simba yaicharaza Dom Jiji 1-0
Simba yaicharaza Dom Jiji 1-0
Read also