Na mwandishi wetu
Klabu ya soka ya Simba imewaongezea mikataba wachezaji wake nyota wawili, kiungo Yusuph Kagoma aliyeongeza miaka miwili na beki Rushine De Reuck (pichani) aliyeongeza mwaka mmoja.
Taarifa ya wachezaji hao wawili tegemeo kuongeza mikataba yao ilipatikana kwenye vyanzo vya habari vya klabu hiyo ya mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Rushine alijiunga na Simba Julai mwaka jan akitokea klabu ya Mamelodi Sundows ya Afrika Kusini na tayari ameonesha uwezo akiwa mmoja wa wachezaji muhimu katika safu ya ulinzi ya Simba.
Simba inatarajia kumtumia mchezaji huyo kuimarisha safu yake ya ulinzi ili kushiriki vyema kwenye michuano ya ligi kuu nchini Tanzania pamoja na ile ya klabu barani Afrika.
Kwa upande wa Kagoma, mchezaji huyo alijiunga na Simba mwaka 2024 akitokea Singida Black Stars na kuanzia wakati huo, kiwango chake kimeendelea kuwa bora mwaka hadi mwaka.
Kwa sasa Kagoma ni mchezaji tegemeo si kwa timu yake ya Simba tu bali hata kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars, ameendelea kuwa mmoja wa wachezaji muhimu.
Kimataifa Rushine, Kagoma waongeza mikataba Simba
Rushine, Kagoma waongeza mikataba Simba
Related posts
Read also
