London, England
Klabu ya soka ya Tottenham Hotspur ya England inayopambana kujinasua na janga la kushuka daraja inatajwa kumsaka aliyekuwa kocha mkuu wa Olympique de Marseille ya Ufarana, Roberto de Zerbi (pichani).
Taarifa za vyanzo mbalimbali vya habari nchini Uingereza vilieleza kuwa, kocha huyo anatakiwa na tayari mazungumzo yameanza huku habari nyingine zikidai kuwa Spurs ikijinasua na janga la kushuka daraja, De Zerbi atakabidhiwa timu.
Awali Spurs ilihusishwa na mipango ya kumtaka De Zerbi mwaka 2023 lakini mpango huo haukufanikiwa na badala yake timu hiyo ikampa kibarua hicho Ange Postecoglou.
Habari za sasa zimezidi kupata nguvu baada ya De Zerbi ambaye pia aliwahi kuinoa Brighton, kuachana na Marseille inayoshiriki Ligi 1 ya Ufaransa ambayo hivi karibuni ilipokea kichapo cha mabao 4-0 mbele ya mahasimu wao Paris Saint-Germain (PSG).
Wakati De Zerbi akiachana na Marseille, Spurs nayo imemtimua kocha Thomas Frank, uamuzi ambao umefikiwa kutokana na mwendelezo wa vipigo ambavyo timu hiyo imekuwa ikikutana navyo kikiwamo kipigo cha mabao 2-1 mbele ya Newcastle.
Kipigo hicho ambacho ni cha saba msimu huu kwenye uwanja wake wa nyumbani kimezidi kuiweka Spurs mahali pabaya na sasa ina tofauti ya pointi tano kati ya timu zinazohaha kujinasua na janga la kushuka daraja.
Kocha mwingine ambaye jina lake pia linatajwa Spurs ni kocha wa zamani wa timu hiyo, Mauricio Pochettino ambaye kwa sasa anainoa timu ya taifa ya Marekani inayojiandaa kwa fainali za Kombe la Dunia 2026.
Kupatikana kwa Pochettino ni wazi kwamba itakuwa baada ya fainali hizo zitakazoanza miezi mitatu ijayo ambapo Marekani ni moja wa timu mwenyeji.
Kimataifa Jina la De Zerbi latajwa Spurs
Jina la De Zerbi latajwa Spurs
Related posts
Read also
