Na mwandishi wetu
Timu ya Yanga imefuzu hatua ya fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa kuichapa Singida Black Stars bao 1-0 katika mechi iliyochezwa Ijumaa Januari 9, 2026 kwenye dimba la New Amaan Complex, Zanzibar.
Bao hilo pekee lililoipa Yanga ushindi lilifungwa na Maxi Nzengeli katika dakika ya 54 baada ya kuinasa pasi ndefu ya Pacome Zouzoua na kuujaza mpira wavuni.
Singida BS baada ya kufungwa bao hilo waliendelea kuonesha umahiri wao wakisaka bao lakini juhudi zao zilishindwa kupenya mbele ya safu ya ulinzi ya Yanga.
Mechi hiyo ilikuwa ya vuta nikuvute kwa timu zote kiasi cha kusababisha kila timu ipoteze mchezaji mmoja uwanjani kwa kupewa kadi nyekundu kutokana na kucheza rafu.
Hali hiyo iliifanya kila timu ibaki na wachezaji 10 uwanjani, kwa Yanga alitolewa Mohamed Damaro na kwa upande wa Singida BS janga hilo lilimkuta, Morice Chukwu.
Kwa ushindi huo Yanga itaumana na Azam FC katika mechi ya fainali ambayo imepangwa kuchezWa Januari 13 kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba.
Soka Yanga yaibwaga Singida BS
Yanga yaibwaga Singida BS
Read also
