Na mwandishi wetu
Kocha mpya wa Simba, Steve Barker ameonja machungu ya kufungwa mara ya kwanza baada ya timu yake kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kupokea kichapo cha bao 1-0 mbele ya Azam FC.
Katika mechi hiyo iliyopigwa Alhamisi Januari 8, 2026, bao pekee lililoizamisha Simba lilifungwa na Lameck Lawi katika dakika ya 73 na kuwaondoa Simba mashindanoni.
Matokeo hayo ni pigo la kwanza kwa Barker ambaye amejiunga na Simba Desemba mwaka jana akitokea Stellenbosch ya Afrika Kusini na hadi sasa tayari ameiongoza timu hiyo katika mechi tatu na kati ya hizo ameshinda mbili.
Wakati Simba ikiaga kwneye Kombe la Mapinduzi, Azam imefuzu hatua ya fainali ya michuano hiyo ya kila mwaka na sasa inasubiri kucheza mechi ya fainali dhiddi ya mshindi wa mechi kati ya Yanga na Singida Black Stars.
Barker amekabidhiwa jukumu la kuinoa Simba baada ya kutimuliwa kwa Dimitar Pantev, bado ana kibarua kingine kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika katika hatua ya makundi pamoja na Ligi Kuu NBC.
Simba sasa inarejea Dar es Salaam ikijiandaa kwa ligi kuu wakati kwenye ligi ya mabingwa itakuwa na kibarua Januari 23 mwaka huu dhidi ya Esperance ya Tunisia.
Soka Azam yaiadhibu Simba
Azam yaiadhibu Simba
Read also
