Na mwandishi wetu
Hatimaye klabu ya soka ya Simba imemtangza rasmi Steve Barker au Steve B (pichani) kuwa kocha mkuu wa timu hiyo ikiwa ni wiki kadhaa zimepita baada ya kutimuliwa kwa Dimitar Pantev.
Steve B ambaye kabla ya kutua Simba alikuwa akiinoa timu ya Stellenbosch inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini anakabidhiwa jukumu la kuinoa Simba baada ya mambo kwenda kombo chini ya Pantev.
Pantev alitimuliwa Desemba 2 mwaka huu ikiwa ni takriban miezi miwili imepita tangu apewe jukumu hilo na ingawa Simba walimtangaza kama meneja wa timu lakini inadaiwa alikuwa akifanya kazi ya kocha mkuu akisaidiwa na Seleman Matola.
Ujio wa Steve B unakuwa umezima minong’ono iliyotawala katika siku za karibuni kuhusu nani hasa angebeba jukumu hilo tangu kutimuliwa kwa Pantev ambaye alishindwa kufikia matumaini ya mashabiki wa timu hiyo.
Pantev alikabidhiwa jukumu hilo kutoka kwa Fadlu Davids lakini mwenendo wa Simba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi umekuwa si wa kuridhisha baada ya timu kupoteza mechi mbili za hatua ya makundi.
Steve B ni kocha mwenye heshima Afrika Kusini kutokana na mafanikio aliyojipatia akiwa na Stellenbosch, timu iliyoanzishwa mwaka 2016 na ni yeye aliyeipandisha ligi kuu nchini humo mwaka 2019.
Mwaka jana Steve B aliifikisha timu hiyo nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na sasa amekabidhia jukumu la kuifundidha Simba bila shaka akibeba matumaini ya kuendelea alipoishia Fadlu Davids.
Soka Steve B kocha mkuu mpya Simba
Steve B kocha mkuu mpya Simba
Related posts
Read also
