Madrid, Hispania
Mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Kylian Mbappe ambaye ni majeruhi ana hatihati ya kucheza mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Man City itakayopigwa Jumatano hii Novemba 10, 2025 baada ya kukosa mazoezi.
Hali hiyo inazidi kuongeza janga la wachezaji majeruhi kwenye kikosi cha Madrid na hivyo kuzidi kumuongezea presha kocha Xabi Alonso ambaye kwa sasa anapitia kipindi kigumu.
Jumanne asubuhi Mbappe hakuonekana kwenye uwanja wa mazoezi wa timu hiyo wa Valdebebasna hivyo kuongeza hofu kuhusu wachezaji wa kikosi cha kwanza wa timu hiyo ambao wataikosa mechi na Man City ambayo Madrid watakuwa nyumbani Bernabeu.
Habari zaidi zinadai kwamba Mbappe ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa, alikuwa afanyiwe vipimo Jumanne jioni kujua undani wa maumivu yanayomkabili na kujua kama atakuwa fiti kuikabili Man City.
Madrid inajiandaa na mechi dhidi ya Man City ikiwa baada ya Jumapili iliyopita kulala kwa mabao 2-0 mbele ya Celta Vigo katika mechi ya La Liga, mechi ambayo pia Mbappe aliumia kidole huku timu hiyo ikiwa imepata ushindi mmoja katika mechi tano zilizopita.
Kwa vyovyote itakavyokuwa matokeo yoyote mabaya katika mechi na Man City yanaweza kuwa sababu mojawapo ya mabosi wa Madrid kuchukua uamuzi wa kumfukuza kazi Alonso.
Kiwango cha Mbappe katika safu ya ushambuliaji ni mingoni mwa mambo yanayoangaliwa zaidi wakati huu mwenendo wa timu ukiwa vibaya, mshambuliaji huyo hadi sasa ana mabao 16 ya La Liga na tisa ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Ukiacha Mbappe, wachezaji wengine wa Madrid ambao tayari ni majeruhi ni mabeki David Alaba, Dani Carvajal, Éder Militão, Ferland Mendy, Dean Huijsen na Trent Alexander-Arnold pamoja na kiungo Eduardo Camavinga.
Kimataifa Mbappe hatihati kuivaa City
Mbappe hatihati kuivaa City
Read also
