Na mwandishi wetu
Simba imekutana na kipigo cha kwanza katika Ligi Kuu NBC baada ya kulala kwa mabao 2-0 mbele ya Azam FC katika mechi iliyopigwa Jumapili Novemba 7, 2025 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
MAtokeo hayo mabaya yamekuja ikiwa ni siku chache zimepita tangu timu hiyo iachane na kocha wake, Dimitar Pantev baada ya kufanya vibaya katika mechi mbili za hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba kwa sasa ipo chini ya kocha Suleiman Matola ambaye amekabidhiwa jukumu hilo na katika mechi yake hiyo ya kwanza mambo yamekwenda vibaya.
Simba ilionesha uhai na kujengeka matumaini ya timu hiyo kuendeleza wimbi la ushindi katika ligi hiyo lakini kadri muda ulivyokwenda ndivyo mapungufu ya timu hiyo yalipojidhihirisha.
Baada ya kushambuliana mara kadhaa huku kila timu ikitaka kulandika bao la kwanza, kasi hiyo iliendelea kwa kipindi chote cha kwanza na timu kwenda mapumziko zikiwa hazijafungana kabla ya mambo kuiharibikia Simba katika kipindi cha pili.
Azam waliandika bao la kwanza dakika ya 81 mfungaji akiwa ni Japhet Kitambala aliyeuwahi mpira katika eneo la hatari na kufumua shuti lililojaa wavuni.
Simba wakionekana kushtushwa na bao hilo la jioni walipambana lakini kwa mara nyingine nyota ya Azam ndiyo iliyong’ara baada ya timu hiyo kuandika bao la pili na la ushindi lililofungwa na Idd Nado katika dakika ya 89.
Soka Azam yairarua Simba 2-0
Azam yairarua Simba 2-0
Read also
