Na mwandishi wetu
Yanga ikiwa ugenini Algeria imefanikiwa kugawana pointi na wenyeji wao JS Kabylie katika mechi ya Kundi B ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyochezwa Ijumaa Novemba 28, 2025 na kumalizika kwa matokeo ya 0-0.
Kelele za mashabiki wa Kabylie zilizosikika mwanzo hadi mwisho wa mchezo hazikuweza kuiyumbisha Yanga ambayo wachezaji wake walicheza kwa kujiamini na kufanya mashambulizi mara kadhaa kwenye lango la wapinzani wao.
Kwa JS Kabylie waliokuwa nyumbani, nao juhudi zao za kusaka bao la nyumbani zilionekana mara kwa mara lakini zilikwamisha na safu imara ya ulinzi iliyoongozwa na kipa Djigui Diarra.
Kwa matokeo hayo Yanga sasa imefikisha pointi nne na ndiyo inayoshika usukani katika kundi hilo ambalo pia lina timu za FAR Rabat ya Morocco na Al Ahly ya Misri, timu ambazo zitatoana jasho Jumamosi.
Nao wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Azam FC mambo yalizidi kuwa mabaya baada ya kulala kwa bao 1-0 mbele ya Wydad AC ya Morocco.
Kwa Azam hicho kinakuwa kipigo cha pili kwa timu hiyo katika michuano hiyo msimu huu, jambo ambalo kwa mara nyingine linaibua wasiwasi kama timu hiyo itafika mbali msimu huu.
Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye dimba la New Amaan, Zanzibar, bao pekee lililoizamisha Azam lilipatikana dakika ya 57 mfungaji akiwa Nordin Amrabat baada ya kuiwahi krosi ya Thembinkosi Lorch.
Katika mechi hiyo nyota wa zamani wa Yanga ambaye kwa sasa anaichezea Wydad, Stephane Aziz Ki alilazimika kukimbizwa hospitali baada ya kuumia.
Kimataifa Yanga yavuna pointi Algeria
Yanga yavuna pointi Algeria
Read also
