Na mwandishi wetu
Jina la mshambuliaji Kelvin John limo katika orodha ya wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars watakaocheza mechi ya kirafiki na timu ya taifa ya Kuwait wakiwa chini ya kocha mpya Miguel Gamondi.
Kelvin (pichani) anayecheza soka la kulipwa nchini Denmark amekuwa mjadala katika siku za karibuni baada ya aliyekuwa kocha wa Stars, Hemed Suleiman ‘Morocco’ kutomwita katika kikosi hicho katika siku za karibuni.
Kitendo cha Morocco kutomwita mchezaji huyo kimekuwa kikizua mjadala hasa kwenye mitandao ya kijamii hali ambayo pia imejidhihirisha baada ya orodha ya wachezaji wa timu hiyo kutangazwa na TFF huku jina la mchezaji huyo likijumuishwa.
Kwa mujibu wa taarifa ya TFF iliyopatikana leo Alhamisi Novemba 5, 2025, wachezaji hao wa Stars chini ya kocha Gamondi wataingia kambini Jumatatu ijayo kujiandaa na mechi na Kuwaita ambayo itachezwa Novemba 14 nchini Misri.
Orodha ya wachezaji hao na timu wanazocheza katika mabano wakiwamo wanaocheza nje ya Tanzania ni Yakoub Suleiman (Simba), Hussein Masalanga (Singida BS), Zubeir Foba (Azam FC), Bakari Mwamnyeto (Yanga) Shomari Kapombe (Simba) na Mohamed Hussein (Yanga).
Wengine ni Alphonce Mabula (Shamakhi-Azerbaijan), Mudathir Yahya (Yanga), Wilson Nangu (Simba), Novatus Dismas (Goztepe FC-Uturuki), Paschal Msindo (Azam FC), Ibrahim Abdullah (Yanga), Feisal Salum (Azam FC) na Haji Mnoga (Salford City-England).
Wachezaji wengine ni Dickson Job (Yanga), Habib Iddi (Singida BS), Tarryn Allarakhia (Rochdale FC-England), Charles M’mombwa (Floriana FC-Malta), Suleiman Mwalimu (Simba), Abdul Suleiman (Azam FC), Morice Abraham (Simba), Paul Peter ((JKT Tanzania) na Kelvin John (Aalborg BK-Denmark).
Kimataifa Kelvin John ndani Stars ya Gamondi
Kelvin John ndani Stars ya Gamondi
Read also
