Na mwandishi wetu
Kocha wa Singida Black Stars ambaye pia amewahi kuwa kocha wa Yanga, Miguel Gamondi ameteuliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars akichukua nafasi ya Hemed Suleiman ‘Morocco’.
Uteuzi huo umetangazwa Jumanne, Novemba 4, 2025 kupitia taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikielezwa kuwa Gamondi kwa sasa atakaimu nafasi hiyo mpya.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyosainiwa na ofisa habari na mawasiliano wa TFF, Clifford Ndimbo, mkataba wa Morocco umesitishwa baada ya makubaliano ya pande mbili yaani TFF na upande wa kocha huyo.
Wakati huo huo mazungumzo tayari yamefanyika baina ya TFF na klabu ya Singida BS kuhusu kocha Miguel kuanza kufanya kazi hiyo mpya.
TFF pia katika taarifa hiyo wameweka wazi kuwa kocha Gamondi ndiye atakayekiongoza kikosi cha Taifa Stars kwenye fainali za michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) zitakazofanyika nchini Morocco kuanzia Desemba mwaka huu.
Gamondi ambaye hivi karibuni ameiwezesha Singida BS kubeba taji la Cecafa na kuifikisha hatua ya makundi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, pia ndiye atakayeiongoza Taifa Stars nchini Misri kwenye michezo ya kirafiki ya kalenda ya Fifa.
Kimataifa Gamondi amrithi Morocco Taifa Stars
Gamondi amrithi Morocco Taifa Stars
Read also
