Na mwandishi wetu
Simba imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Namungo FC katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyochezwa Jumatano hii Oktoba Mosi, 2025 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Simba walianza kuandika bao lao la kwanza dakika mbili kabla ya mapumziko mfungaji akiwa ni Chamou Karaboue ambaye alifunga kwa kichwa akimalizia mpira wa kona iliyochongwa na Joshua Mutale.
Simba waliongeza bao la pili dakika ya 60, bao lililofungwa na Rushine De Reuck ambaye pia ndiye aliyeibuka mchezaji bora wa mechi hiyo, De Reuck alifunga bao hilo akimalizia mpira uliopigwa na Neo Maema.
Karamu ya mabao ya Simba ilikamilishwa na Suleiman Mwalim aliyefunga bao la tatu dakika ya 83 baada ya kumlamba chenga mlinzi mmoja wa Namungo na kuujaza mpira wavuni kwa shuti la mguu wa kushoto lililomshinda malinda mlango, Jonathan Nahimana.
Mambo yalianza kuwaendea ndivyo sivyo Namungo, mapema dakika ya 10 ya mchezo baada ya mshambuliaji wao tegemeo, Haritie Makambo kupata maumivu na nafasi yake kuingia Fabrice Ngoy.
Mabadiliko hayo hayakuweza kuisaidia timu hiyo kupata bao na hadi mwisho wa mchezo Simba walitoka kifua mbele na moja kwa moja kushika usukani wa ligi wakiwa na pointi sita na mabao sita.
Soka Simba yaipa Namungo dozi ya 3-0
Simba yaipa Namungo dozi ya 3-0
Read also
