Na mwandishi wetu
Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Hemed Suleiman ‘Morocco’ ametangaza kikosi cha wachezaji 26 wa timu ya taifa kwa ajili ya mechi na Zambia huku akiwaacha wachezaji wakongwe wa timu hiyo.
Miongoni mwa wakongwe ambao mara kadhaa majina yao hayakosekani lakini safari hii wameachwa ni nahodha Mbwana Samatta, Simon Msuva, Shomari Kapombe, Mudathir Yahya, Kibu Dennis na Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’.
Uamuzi wa Morocco kuwaacha wachezaji hao huenda una nia ya kuwapa nafasi wachezaji wengine hasa kwa kuwa matokeo ya mechi dhidi ya Zambia ambayo ni ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 hayawezi kuibeba timu hiyo.
Katika orodha hiyo iliyopatikana Jumatano Oktoba Mosi, 2025, wachezaji walioitwa ni makipa Yakoub Suleiman wa Simba, Zuberi Foba wa Azam FC na Hussein Masalanga wa Singida BS.
Wachezaji wengine na timu zao kwenye mabano ni Ibrahim Abdullah ‘Bacca’ (Yanga), Lusajo Mwaikenda (Azam fC), Bakari Mwamnyeto (Yanga), Elias Lawi (Azam FC), Israel Mwenda (Yanga), Wilson Nangu (Simba), Novatus Dismas (Goztepe FC) na Paschal Msindo (Azam FC).
Wengine ni Dickson Job (Yanga), Haji Mnoga (Salford City), Offen Chikola (Yanga) Miano Danilo (FK Panevezys), Aziz Andabwile (Yanga), Yahya Zaid (Azam FC), Yusuf Kagoma (Simba), Habib Idd (Singida BS), Tarryn Alarakhia (Rochdale AFC) na Charles M’mombwa (Floriana FC).
Katika orodha hiyo pia wamo Feisal Salum (Azam FC), Suleiman Mwalim (Simba), Morrice Abraham (Simba), Edwin Balua (EN Paralimniou) na Abdul Suleiman (Azam FC).
Kimataifa Kocha Stars awaacha wakongwe
Kocha Stars awaacha wakongwe
Read also
