Na mwandishi wetu
Uongozi wa klabu ya Simba na Kampuni ya Jayrutty Investment umebaini kuwapo kwa jezi feki katikaza Simba mikoa ya Morogoro, Singida, Mwanza na Geita.
Kwa mujibu wa taarifa ya klabu ya Simba ugunduzi wa jezi hizo feki umetokana na opertesheni maalum ambayo imefanywa kwa ushirikiano kati ya klabu hiyo na polisi na tayari baadhi ya watuhumiwa wamekamatwa na wanatarajia kuchukuliwa hatua za kisheria.
Katika taarifa hiyo, Simba wamebainisha kuwa uzalishaji, uuzaji, usambazaji na utumiaji wa jezi ambazo hazijazalishwa na Jayrutty ni kosa kisheria na hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika.
“Hatua zitachukuliwa kwa yeyote atakayethubutu kuzalisha, kuuza, kusambaza ama kutumia jezi na bidhaa feki kwani vitendo hivyo ni uhujumu wa wazi dhidi ya klabu ya Simba,” ilieleza taarifa hiyo.
Simba pia wameahidi kuweka ulinzi mkali kote Tanzania kwa lengo la kudhibiti na kukamata wahusika wote wa bidhaa feki na kuwataka wanasimba na raia wote kutoshiriki katika matumizi ya bidhaa feki.
Katika taarifa hiyo, Simba na Jayrutty pia wametaka mtu yeyote atakayebaini uwepo wa jezi na bidhaa feki mahala popote atoe taarifa kituo chochote cha polisi au apige simu namba, 0752 111 181 au 0784 128 220 na 0742 771 311.
Simba kwa kushirikiana na Jayrutty pia wameahidi zawadi nono kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazofanikisha kukamatwa kwa wazalishaji, wasambazaji, wauzaji na watumiaji wa jezi feki.
Hakimiliki Simba wabaini jezi feki
Simba wabaini jezi feki
Read also
