Na mwandishi wetu
Shiriklsho la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya waamuzi 29 kwa ajili ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) wakiwamo waamuzi watatu wa Tanzania.
Waamuzi hao kutoka Tanzania ni Ahmed Arajiga ambaye ni mwamuzi wa kati pamoja na waamuzi wasaidizi wawili, Ally Hamdani Said na Frank John Komba.
Kuchomoza kwa jina la Arajiga ni mafanikio mengine kwa mwamuzi huyo ambaye pia amewahi kupewa nafasi ya kuchezesha mechi kadhaa za kimataifa zikiwamo zile za Fifa.
Tanzania, Kenya na Uganda watakuwa wenyeji wa michuano hiyo itakayoanza Agosti 2 mwaka huu huku waamuzi wawili kutoka Kenya wakiteuliwa na CAF kama ilivyo kwa Uganda.
Nchi nyingine zilizotoa waamuzi katika fainali hizo ni Algeria, Morocco na Burkina Faso ambazo ni nchi pekee zilizotoa waamuzi wa kati wawili wawili kwa kila nchi.
Sambamba na nchi hizo, nchi nyingine ambazo waamuzi wake wamo kwenye orodha ya CAF ni Senegal, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Cameroon, Zimbabwe, Ivory Coast, Mali na Madagascar.
Timu shiriki zitakuwa katika makundi manne ambapo Kundi A mechi zake zitachezwa jijini Nairobi, Kenya, Kundi B ni Dar es Salaam, Tanzania wakati Kundi C ni Kampala Uganda na Kundi D ni Zanzibar.
Soka CAF yamteua Arajiga CHAN
CAF yamteua Arajiga CHAN
Read also
