Na mwandishi wetu
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza kufunguliwa kwa maombi ya leseni ya klabu za ligi kuu kwa wanaume na wanawake pamoja na ligi ya Championship kwa msimu mpya wa 2025-26.
Taarifa ya TFF iliyosainiwa na ofisa habari na mawasiliano wa shirikisho hilo Cliford Ndimbo ilieleza kuwa maombi hayo yatafanyika kwa njia ya mtandao kuanzia Julai 14, 2025.
Waombaji wamekumbushwa kuwa mwisho wa kuwasilisha maombi hayo itakuwa ni Agosti 15, 2025 na yatawasilishwa kupitia mtandao https://clop.cafonline.com.
Katika taarifa hiyo, klabu zimetakiwa kuwasilisha myaraka na taarifa zote kwa wakati kwani hakutakuwa na muda wa ziada baada ya dirisha la maombi kufungwa.
TFF pia imetahadharisha kuwa klabu yoyote ambayo itakuwa inadaiwa na mchezaji haitopewa leseni ya kushiriki ligi.
Kuhusu klabu zinazoshiriki mashindano yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), TFF imefafanua kuwa kocha wa timu hiyo lazima awe na Diploma A ya CAF wakati msaidizi wake anatakiwa kuwa na Diploma B pia ya CAF.
Soka TFF yaziita klabu kuomba leseni
TFF yaziita klabu kuomba leseni
Read also
