Madrid, Hispania
Polisi nchini Hispanai wamesena kuwa kifo cha mchezaji wa Liverpool, Diogo Jota (pichani) huenda kilitokana na kuendesha gari kwa mwendo wa kasi.
Jota, 28, na kaka yake walifariki juma lililopita kwa ajali ya gari, msiba ambao umegusa hisia za watu mbalimbali duniani kote hususan mashabiki wa soka.
Kwa mujibu wa polisi, ingawa uchunguzi wa ajali na kifo hicho unaendelea, wanaamini Jota alikuwa akiendesha gari lake la kifahari aina ya Lamborghini kwa kasi kabla ya tairi kupasuka.
Awali mara baada ya ajali hiyo, taarifa ya polisi haikusema kama Jota au kaka yake, Andre Silva mmoja wao alikuwa akiendesha gari hilo, lakini sasa wamesema inaonekana ni Jota ndiye aliyekuwa dereva.
Ndugu hao wawili walikufa wakiwa kwenye gari hilo ambalo lilipasuka tairi na kuwaka wakiwa katika barabara kubwa majira ya asubuhi.
Vyombo vya habari nchini Ureno anakotoka mchezaji huyo viliripoti kuwa Jota, alikuwa akielekea Kaskazini mwa Hispania katika mji wa Santander kwa ajili ya kujiandaa na safari ya England kuungana na wachezaji wenzake wa Liverpool.
Ndugu hao walizikwa Jumamosi ya Julai 5, 2025 katika mji wa Condomar nchini Ureno, mji ambao ndiko wawili hao walipokulia.
Kimataifa Mwendo kasi watajwa kifo cha Jota
Mwendo kasi watajwa kifo cha Jota
Related posts
Read also
