Madrid, Hispania
Watu wanne wamekutwa na hatia ya kosa la kumdhihaki mshambuliaji wa Real Madrid, Vinicius Jr ‘Vini Jr’ kwa kutumia sanamu linalotumika kuvutia wateja kwenye maduka ya nguo.
Katika kosa hilo ambalo ni la jinai, watu hao wanadaiwa Januari 2023 waliweka sanamu hilo likiwa la mfano wa mchezaji huyo kwenye daraja moja karibu na uwanja wa mazoezi wa Real Madrid.
Watu hao wanadaiwa kufanya kosa hilo muda mfupi kabla ya kuanza kwa mechi ya Copa Del Rey kati ya Real Madrid na Atletico Madrid iliyopigwa kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.
Sanamu hilo lilikuwa na maandishi yaliyosomeke Madrid wanaichukia Real na katika adhabu waliyopewa, watatu walihukumiwa kifungo cha miezi 14 jela wakati mwingine alipewa kifungo cha miezi 22 kwa kosa la kusambaza picha za sanamu hilo mitandaoni.
Adhabu hiyo hata hivyo imebadilishwa na kuwa kifungo cha nje baada ya washitakiwa wote wanne kuandika barua ya kuomba msamaha kwa Vinicius, klabu ya Real Madrid, mamlaka za Ligi Kuu Hispania au La Liga na Shirikisho la Soka Hispania.
Adhabu hiyo sasa inawataka washitakiwa kuhakikisha wanakuwa umbali wa kilometa moja mahali alipo Vini Jr, nyumbani kwake au kwenye uwanja wa Real Madrid pamoja na kufungiwa moja kwa moja kuhudhuria mechi za La Liga au timu ya taifa ya Hispania.
Vini Jr amekuwa mhanga wa matukio ya ubaguzi wa rangi tangu ajiunge na Real Madrid mwaka 2018 akitokea Flamengo ya Brazil.
Kimataifa Wanne hatiani kwa kumdhihaki Vini Jr
Wanne hatiani kwa kumdhihaki Vini Jr
Read also
