London, England
Klabu ya Newcastle United imekubali kumsainisha winga Anthony Elanga (pichani) kutoka Nottingham Forest kwa ada ya Pauni 55 milioni.
Newcastle imedhamiria kuimarisha safu yake ya ushambuliaji wakati huu ikijinoa kurudi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kumaliza nafasi ya tano kwenye Ligi Kuu England (EPL) msimu uliopita.
Elanga, 23, ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Sweden, amefunga mabao sita na kutoa asisti 11 katika kikosi cha Forest msimu wa 2024-25.
Kwa kipindi hiki cha usajili majira ya kiangazi, Newcastle haijalipa ada ya usajili kwa mchezaji yeyote, mchezaji pekee mpya aliyejiunga na timu hiyo ni winga mwenye miaka 18, Antonio Cordero kutoka Malaga aliyesajiliwa akiwa mchezaji huru.
Usajili wa Elanga kwenda Newcastle inakuwa biashara nzuri kwa Forest ambayo ilimnunua mwaka 2023 kutoka Man United kwa ada inayotajwa kufikia Pauni 15 milioni na kumsainisha mkataba wa miaka mitano.
Elanga alijiunga na Man United, akiwa kijana mdogo wa miaka 12 na ameichezea timu hiyo mara 55 kabla ya kuhama.
Kimataifa Newcastle yainasa saini ya Elanga
Newcastle yainasa saini ya Elanga
Read also
