California, Marekani
Bayern Munich imeanza kwa kishindo michuano ya Fifa ya Klabu ya Dunia kwa kuweka rekodi ya ushindi wa mabao 10-0 dhidi ya Auckland City katika mechi iliyochezwa Jumapili hii Juni 15, 2025.
Vinara hao wa Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga waliutawala vyema mchezo huku Jamal Musiala akifunga mabao matatu (hat trick) na Thomas Muller akipachika mawili.
Bayern chini ya kocha Vincent Kompany walianza kuziona nyavu za wapinzani wao kutoka New Zealand katika dakika ya sita ya mchezo kwa bao la Kingsley Coman.
Dakika sita baadaye Bayern waliongeza bao la pili lililofungwa na Sacha Boey kabla Michael Olise hajapahika bao la tatu alipoinasa krosi ya Muller.
Wakati Auckland City wakitafakari, Coman kwa mara nyingine alitupia mpira kambani na kuifanya Bayern ifikishe mabao manne huku yeye akiwa amefunga la pili.
Muda mfupi kabla ya timu kwenda mapumziko, Muller alifunga bao la tano akiitumia krosi ya Olise kabla Olise hajakamlisha bao la sita na kuzifanya timu ziende mapumzko Bayern wakiwa mbele kwa mabao 6-0.
Kasi ya Bayern kupachika mabao ilipungua kidogo kipindi cha pili lakini hatimaye dakika ya 67 Musiala aliongeza bao la saba .
Musiala ambaye alizikosa mechi sita za Bayern za mwishoni mwa msimu kutokana na kuwa majeruhi, aliandika bao la nane kwa mkwaju wa penalti dakika ya 73 na kukamilisha bao lake la tisa na la tatu kwenye mechi hiyo katika dakika ya 84.
Bao la 10 na la mwisho kwa Bayern lilifungwa na Muller zikiwa zimebakia dakika mbili kumalizika kwa mchezo huo.
Ushindi wa Bayern unaingia kwenye rekodi ya kuwa ushindi wa mabao mengi zaidi katika mashindano hayo baada ya ule wa mwaka 2022 wa Al Hilal kuichapa Al Jazira mabao 6-1.
Katika mechi nyingine vinara wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, PSG ya Ufaransa waliilaza Atletico Madrid mabao 4-0 huku mabao ya washindi yakifungwa na Fabián Ruiz,
Vitinha, Mayulu kwa mkwaju wa penalti na Lee Kang-In.
Kimataifa Bayern yashinda 10-0
Bayern yashinda 10-0
Related posts
Read also