Manchester, England
Klabu ya Manchester City inadaiwa kuwa katika hatua nzuri kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Lyon, Rayan Cherki (pichani)kwa ada inayotajwa kufikia Dola 45.5 milioni.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21, Alhamisi iliyopita alionesha uwezo wake katika mechi ya kimataifa wakati akiichezea timu ya taifa ya Ufaransa iliyokuwa ikiumana na Hispania.
Katika makubaliano ya kumsajili mshambuliaji huyo, inadaiwa kwamba atasaini mkataba wa miaka mitano ambao pia utahusisha marupurupu mengine.
Taarifa zaidi zinadai kwamba mshambuliaji huyo huenda leo Jumanne Juni 10, 2025 akafanyiwa vipimo vya afya na matumaini yaliyopo ni kwamba anatarajia kuiwakilisha Man City katika michuano ya Fifa ya Kombe la Dunia la Klabu.
Man City chini ya kocha Pep Guardiola inajiandaa kuweka kambi mjini Florida wakati wowote wiki hii ikijiandaa kwa mechi yao ya kwanza ya michuano hiyo dhidi ya Waydad Casablanca ya Morocco, mechi itakayopigwa Juni 18 mjini Philadelphia.
Cherki amekuwa akiwaniwa na klabu kadhaa za England na Ujerumani lakini Pep ndiye anayetajwa kufanikiwa kumpata mshambuliaji huyo baada ya mazungumzo ya wawili hao.
Akiwa na Lyon, Cherki ameifungia timu hiyo mabao 29 katika mechi 185 na uhamisho wake ukikamilika atakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Man City katika kipindi hiki cha usajili wa Majira ya Kiangazi.
Kimataifa Cherki mbioni kutua Man City
Cherki mbioni kutua Man City
Related posts
Read also