Na mwandishi wetu
Wachezaji wa timu ya taifa ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’ wanaingia kambini leo Jumatatu Juni 2, 2025 kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya kirafiki na timu ya Afrika Kusni ‘Bafana Bafana’.
Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, wachezaji hao chini ya kocha Hemed Suleiman ‘Morocco’ (pichani) na timu wanazotoka katika mabano ni Yakoub Suleiman (JKT Tanzania), Ally Salim (Simba), Hussein Msaranga (Singida BS) na Anthony Remmy (Azam FC U-20).
Wengine ni Shomary Kapombe (Simba) Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Vedastus Masinde (TMA Stars), Wilson Nangu (JKT Tanzania), Mohamed Hussein (Simba), Ibrahim Ame (Mashujaa) na Paschal Msindo (Azam FC),
Wachezaji wengine ni Alphonce Mabula (Shamakhi FC), Ibrahim Abdullah (Yanga), Dickson Job (Yanga), Abdulrahim Bausi (JKT Tanzania), Idrissa Stambuli (Mashujaa), Abdulrazack Mohamed (Simba), Ahmed Pipino (KMC) na Yusuph Kagoma (Simba).
Wengine ni Shekhan Hamis (Yanga), Feisal Salum (Azam FC), Valentino Mashaka (Simba), Kibu Denis (Simba), Saimon Msuva (Al Talaba SC), Idd Seleman (Azam FC), Mishano Daud (Ken Gold) na Seleman Mwalimu (Wydad Casablanca).
Timu hiyo mbali na kucheza na Bafana Bafana pia itashiriki michuano ya Cosafa kwa kucheza na timu za Eswatini na Madagascar.
Kimataifa Wachezaji Stars waingia kambini
Wachezaji Stars waingia kambini
Read also
