Na mwandishi wetu
Yanga imetua hatua ya fainali Kombe la Shirikisho CRDB baada ya kuinyuka JKT Tanzania mabao 2-0 katika mechi ya nusu fainali iliyochezwa leo Jumapili, Mei 18, 2025 kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani, Tanga.
Yanga ilianza kuhesabu bao la kwanza dakika nne kabla ya timu kwenda mapumziko mfungaji akiwa ni Prince Dube aliyefumua shuti lililomshinda kipa wa JKT, Yakub Suleiman.
Bao la pili la Yanga lilifungwa na kiungo Mudathir Yahya katika dakika ya 90 akiitumia pasi ya Clatous Chama.
JKT pamoja na kipigo hicho lakini walionesha uhai kwa dakika zote 90 kwa kupeleka mashambulizi mara kadhaa kwenye lango la Yanga lakini safu ya ulinzi ya timu hiyo wakati wote ilikuwa kikwazo.
Hii ni mara ya tano mfululizo kwa Yanga kufika hatua ya fainali ya michuano hiyo na sasa inasubiri kuumana na mshindi wa mechi nyingine ya nusu fainali kati ya Simba na Singida Black Stars, mechi iliyopangwa kuchezwa Mei 31 mjini Manyara.
Soka Yanga yafuzu fainali Shirikisho CRDB
Yanga yafuzu fainali Shirikisho CRDB
Read also