Barcelona, Hispania
Mshambuliaji wa Man United, Marcus Rashford inadaiwa yuko tayari na anaufurahia mpango wa kusajliwa Barcelona au Barca kwa makubaliano ya kupunguziwa mshahara.
Rashford, 27, kwa sasa anaichezea Aston Villa kwa mkopo lakini amevutiwa na shauku ya Barca kuitaka huduma yake mara baada ya msimu huu katika dirisha kubwa la usajili Majira ya Kiangazi.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari inadaiwa kuwa nia ya Barca ni kumchukua mchezaji huyo kwa mkopo kwanza na baadaye kuweka mazingira ya kumsajili moja kwa moja kwa kumpa mkataba wa kudumu.
Rashford aliamua kuondoka Man United na kutua Aston Villa kwa mkopo baada ya mambo yake kutokuwa mazuri kwa kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Kabla ya kuondoka kocha wa Man United, Ruben Amorim alimpa uhuru wa kuamua kuondoka wakati wowote akiona inafaa jambo ambalo mchezaji huyo aliliridhia kwa kujiunga Aston Villa kwa mkopo.
Kimataifa Rashford avutiwa kwenda Barca
Rashford avutiwa kwenda Barca
Read also