Na mwandishi wetu
Simba kesho Ijumaa Mei 2, 2025 itaikabili Mashujaa FC katika mechi ya Ligi Kuu NBC itakayopigwa kwenye Uwanja wa KMC huku Simba wakionesha dalili zote za kuipania mechi hiyo.
Akizungumza kupitia vyanzo vya habari kwa klabu ya Simba, kocha msaidizi wa timu hiyo, Suleiman Matola alisema mechi hiyo kwao ni kama fainali na kwamba wamejiandaa vya kutosha.
Matola alisema kwamba Simba wanatambua ubora wa mpinzani wao lakini wanaamini wao watakuwa bora zaidi na kwenda kuchukua pointi tatu kama malengo yao yalivyo.
Naye kiungo wa timu hiyo, Awesu Awesu alisema morali ya wachezaji wote ipo juu kwa ajili ya kupata ushindi kwenye mechi hiyo ambayo wanaipa uzito ili kucheza vizuri na kupata pointi tatu.
Simba ambayo pia inashiriki Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa imefuzu hatua ya fainali, kwa sasa imerudi kwenye Ligi Kuu NBC ikiwa nafasi ya pili ikianza mapambano ya kumuengua kileleni hasimu wake Yanga.
Yanga inashika usukani ikiwa na pointi 70 katika michezo 26 huku Simba ikiwa na pointi 57 katika michezo 22 wakati Mashujaa yenyewe ipo nafasi ya 10 na pointi zake 30 ikiwa imecheza mechi 26.
Soka Simba waisubiri Mashujaa kwa hamu
Simba waisubiri Mashujaa kwa hamu
Read also
